Mchezaji kiraka wa klabu ya Simba, Erasto Nyoni anatarajiwa kuungana na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ''Taifa Stars'' mwishoni mwa wiki hii nchini Cameroon kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.
Nyoni hakuwepo kambini wakati Taifa Stars ikijiandaa na michuano hiyo kwakuwa alielekea nyumbani kwao mkoani Ruvuma kutatua matatizo ya kifamilia lakini alishindwa kurejea kikosini kwa wakati.
Taifa Stars iliondoka nchini alfajiri jana na kuwasili Cameroon tayari kwa matayarisho ya mwisho ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kesho Januari 16, 2021.
Tanzania itaanza kampeni zake za kuwania kufika mbali katika michuano hiyo ikitokea kundi D kwa kukipiga dhidi ya Zambia Januari 19 mwaka huu.
0 Comments