IMEELEZWA kuwa Bernard Morrison nyota wa kikosi cha Simba atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na matatizo ya kiafya.
Nyota huyo amekuwa hana nafasi ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuibukia huko akitokea Klabu ya Yanga ambayo imekuwa ikieleza kuwa bado mchezaji huyo ni mali yao.
Kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliochezwa Uwanja wa Amaan, Januari 13 dhidi ya Yanga alikuwa benchi na alipata muda wa kufanya mazoezi ila hakuingia kucheza.
Timu yake ilipoteza kwa kufungwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sara ya bila kufungana kwa watani hao wa jadi na kufanya ubingwa uende mitaa ya Jangwani.
Taarifa iliyotolewa na Kassim Dewji, Mjumbe wa Bodi ndani ya Simba imeeleza kuwa:"Mchezaji Morrison anaumwa na imeshauriwa aweze kufanyiwa vipimo zaidi ili aweze kurejea ndani ya uwanja.
"Kwa muda mrefu hajawa uwanjani na amekuwa hafanyi mazoezi na wenzake zaidi ya mazoezi mepesi kuna programu ambayo amepewa hivyo mpaka afanyiwe upasuaji atarejea ndani ya uwanja.
"Hajaonekana kwa muda mrefu akicheza hilo lipo wazi na imeshauriwa kuwa akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita ndipo atarejea kwenye ubora wake," ilieleza taarifa hiyo.
0 Comments