TANGAZA NASI

header ads

Miundo mbinu mizuri ya kujifunzia ilivyo ipaisha shule ya Elisabene kushika nafas ya pili Kitaifa darasa saba

 


Na, Baraka Messa, Tunduma

BAADA ya shule ya Elisabene Pre and Primary English Medium School iliyopo katika Halmashaur ya mji Tunduma wilayani Momba Mkoani Songwe kushika nafas ya pili kitaifa matokeo darasa la Saba walimu waeleza miundo mbinu mizur ya kujifunzia ilivyowapaisha mpaka nafas ya hiyo.

Akiongea na mwandishi wa gazeti hili shuleni hapo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo David Buyogela alisema miundo mbinu mizur ya kujifunzia, matumizi mazur ya muda na ushirikiano mzuri wa wazazi na walimu ndio chanzo Cha mafanikio ya shule hiyo iliyo anzishwa mwaka 2014 ikianza na wanafunzi watatu.

Alisema shule hiyo imefanya mtihani wa darasa la Saba  mara ya Kwanza mwaka Jana 2020 nakufanikiwa kushika nafasi ya pili kitaifa .

"Toka 2017 mtihani Taifa wa darasa la nne tumekuwa tukishika nafasi ya Kwanza kimkoa kati ya zaidi ya shule 300 ,na nafas za juu kitaifa, 

kizuri zaidi mwaka Jana ikiwa ni mara ya Kwanza kabisa kutoa wanafunzi wanaomaliza darasa la Saba shule yetu imeshika nafas ya pili kitaifa baada ya matokeo kutoka" alisema Mwalimu Mkuu Buyogela.

Kuhusu idadi ya wanafunzi alisema licha ya kuanza na wanafunzi wachache kutokana na shule hiyo kufanya vizuri kitaaluma idadi imekuwa ikiongezeka na mpaka hivi Sasa kufikia wanafunzi 588

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Aniven Shitindi alisema mafanikio yao yanatokana na kusimamia vema mtaala wa elimu wa Serikali kuanzia vipindi vya masomo, muda wa kazi ,usafi na afya ya wanafunzi .

Alisema lengo lao ni kuhakikisha kuboresha zaidi mazingira ya kujifunzia na kuimalisha ushirikiano Kati ya wazazi, walimu pamoja na Serikali ili kufanikisha lengo la kuwa shule Bora zaidi.

"Matarajio yetu na mipango yetu ni kuhakikisha tunaongoza kwa kushika nafasi ya Kwanza Kitaifa" alisema Shitindi.

Pamoja na mafanikio ya shule yao ya kushika nafas ya pili kitaifa , anazitaja changamoto za ukosefu wa umeme,  maji na barabara kuharibika kipindi mvua kuwapelekea ufanisi kupungua.

"Tunaimani tukisaidiwa huduma ya umeme hapa shuleni mazingira ya kujisomea na kufundisha yataimalika zaidi , kwani mpaka Sasa tunatumia umeme wa solar" aliongeza Shitindi.

Afisa elimu idara ya elimu Msingi Halmashaur ya mji Tunduma Wilson Mtafya alisema uwekezaji katika ujenzi wa shule kwa mji wa Tunduma umeongeka kwa kiasi kikubwa na kuinua taaluma tofauti na miaka ya nyuma ambapo Tunduma ulifahamika kwa biashara zingine tu.

Post a Comment

0 Comments