TANGAZA NASI

header ads

China yaipiku Marekani na kuchukua nafasi ya kwanza kama kivutio cha uwekezaji wa kigeni duniani

 


China imeipiku Marekani kama eneo linalolengwa na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kulingana na takwimu za UN zilizotolewa siku ya Jumapili.

Nusu ya uwekezaji mpya nchini Marekani kutoka katika makampuni ya kigeni ulishuka mwaka uliopita hatua iliosababisha taifa hilo kupoteza nafasi yake ya kwanza.

Kwa upande mwingine, takwimu hizo zinaonyesha uwekezaji wa moja kwa moja katika kampuni za Wachina uliongezeka kwa asilimia 4 , na kulifanya taifa hilo kuchukua nafasi ya kwanza duniani.

Kupanda kwa China kunaonesha ushawishi wake katika sekta ya kiuchumi duniani.

China ilijipatia kipato cha $163bn (£119bn) mwaka uliopita , ikilinganishwa na $134bn zilizoingia Marekani, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maenedeleo (UNCTAD) ulisema katika ripoti yake.

Mwaka 2019, Marekani ilipokea $251bn kupitia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni huku China ikijipatia$140bn.

Huku China ikiwa katika nafasi ya kwanza kwa uwekezaji mpya wa kigeni, Marekani bado inatawala katika uwekezaji wa jumla kutoka mataifa ya kigeni.

Hii inaonyesha miongo ambayo imetumia kama eneo la kuvutia zaidi kwa wafanyabiashara wa kigeni wanaotafuta kupanua biashara zao ng'ambo.

Lakini wataalam wanasema takwimu hizo zinasisitiza hatua ya Uchina kuelekea katikati mwa uchumi wa ulimwengu ambao kwa muda mrefu umetawaliwa na Marekani, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi duniani .

China , kwa sasa inayohusika katika vita vya kibiashara na Marekani , ilitabiriwa kwamba italipiku taifa hilo kufikia 2028, kulingana na kituo cha Utafiti wa kiuchumi na Biashara CBR kutoka Uingereza.

Post a Comment

0 Comments