TANGAZA NASI

header ads

Wakulima,wafanyabiara wa parachichi wakabidhiwa vyeti vya ubora

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wakulima  wa zao la parachichi ambalo limebatizwa jina la Dhahabu ya kijani kutokana na kuongezeka kwa mahitaji yake sokoni,wamesema kitendo cha kituo cha kimataifa cha biashara ITC kuwapa vyeti vya ubora vinavyotambuliwa kimataifa kitawafanya kudhibiti biashara chafu iliyokuwa ikifanywa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani huku ikiwasaidia wakulima na wafanyabiara wa Tanzania kutambuliki kimataifa kutokana na kukidhi vigezo vya uzalishaji.


Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa vyeti vya ubora wawakilishi wa wakulima 600 kutoka kwenye vikundi 8 vya mkoa wa Njombe na kikundi 1 kutoka mkoa wa Mbeya akiwemo Steven Mlimbila,Transit Nyika na Lucy Kilasi wanasema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakihujumiwa na wafanyabishara wa nchi jirani hivyo kitendo cha kituo cha biashara cha kimataifa kuwatambua kinafungua milango kwao kwenda moja kwa moja sokoni .


“Nina imani sasa hivi hata nchi yetu itapanda kwenye nafasi za uuzaji wa zao la parachichi nje kwasababu asilimia kubwa yatatoka yakiwa na nembo ya Tanzania na hatutapitia kibiaashara kwenye nchi za jirani kama awali kwa hiyo sisi wenyewe tutatoka nayo moja kwa moja bila kupitia kwa madalali kwa kuwa walikuwa wanapanga bei wanavyotaka”alisema Stiven Mlimbila mkulima wa zao la parachichi



Aidha kutokana na kukabidhiwa vyeti hivyo wakulima wameshukuru serikali kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika zao hilo na kusababisha kwa sasa kuwa zao la kimkakati huku wakiahidi kushirikiana ili kufikia mafanikio ya kiuchumi kupitia zao hilo.


Safari Fungo ni mratibu wa mradi wa kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara wadogo (MARKUP)  ukanda wa Afrika Mashariki,anayehuhudumia Tannzania,amesema lengo la kuwakabidhi wakulima vyeti hivyo ni kuhakikisha wakulima wanaongeza zaidi thamani na kuuza bidhaa zao katika soko lolote duniani.



“Leo hapa ilikuwa ni hafla ya kuwagawia vyeti wakulima wa parachichi,vyeti vya ubora wa kimataifa vinavyoitwa Global Gap ni vyetu ambavyo vinawawezesha wauze bidhaa zao katika soko lolote duniani.Na tuliangalia vile vikundi ambavyo vzinamahusiano na wauzaji wa nje ya nchi”alisema Safari Fungo


Awali akitoa msimamo wa serikali katika sekta ya kilimo hususani Parachichi mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amesema wataendelea kuweka mazingira rafiki kwa wakulima na wawekezaji  pamoja na kutafuta masoko ya uhakika kwa malighafi zinazozalishwa nchini.


“Ardhi yetu ni nzuri na inarutuba kinachotakiwa ni kuendelea kuzingatia kanuni vizuri za kilimo kwa kuwa parachichi yetu ina thamani kubwa sana.Na sisi serikali wajibu wetu ni kuhamasisha uwekezaji ili tuwe na viwanda vingi”alisema Rubirya


Post a Comment

0 Comments