TANGAZA NASI

header ads

Joe Biden amteuwa Pete Buttigieg kuwa waziri wa usafirishaji



 Rais mteule wa Marekani Joe Biden amemteuwa mpinzani wake wa zamani Pete Buttigieg kuwa waziri wa usafirishaji na ana mpango pia wa kumteua gavana wa zamani wa jimbo la Michigan Jennifer Granholm kuwa waziri wa nishati. 

Aidha katika mipango yake anatarajiwa pia kumchagua Gina McCarthy, mkuu wa zamani wa shirika la Ulinzi wa Mazingira, katika wadhfa wenye nguvu wa ndani, wenye dhamana ya mabadiliko ya ndani ya tabia nchi, ili aweze kushuguhulia mipango yake kabambe ya kimazingira nchini humo. 

Wote watatu watakuwa watajikita katika mipango ya Biden ya kuzifanyia marekebisho sera na miongozo kwa lengo la kupunguza uchafuzi wa mazingira. 

Hatua hiyo ni muendelezo wa Rais Mteule Joe Biden kufanya teuzi zake kabla hajaingia rasmi katika Ikulu yaMarekani Januari 20 mwakani.

Post a Comment

0 Comments