TANGAZA NASI

header ads

Shule Maalum,Mlemavu wa viungo apigwa jeki na mbunge Kamonga Ludewa

 


Na Amiri Kilagalila, Njombe


Wanafunzi wa shule ya elimu maalum ya Mundindi iliyopo kata ya Mundindi Tarafa ya Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameshindwa kuendelea na masomo ya sekondari kutokana na upungufu wa shule zenye mahitaji maalum mkoani humo.


Hayo yalielezwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Amos Mtitu baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kutoka kwa Mbunge wa Ludewa Wakili Joseph Kamonga aliyevitoa kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.



Alisema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifaulu elimu yao ya msingi lakini yanapofanyika machaguo wamekuwa wakipelekwa shule za sekondari za kata ambazo hazina wataalam.


Alisema shule hiyo ina makundi matatu ya wanafunzi wasioona, viziwi na wenye ulemavu wa akili hivyo wanafunzi wanapofaulu wanahitaji walimu ambao wanaweza kuwasiliana nao kwa kwa alama.


"Ukimpeleka mwanafunzi shule ambayo hakuna mwalimu wa alama Wala wa kumuhudumia hivyo akikosa mawasiliano anakata tamaa na kurudi nyumbani" Alisema Amos.


Mwakilishi wa mbunge huyo Stanley Gowele mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo alisema kutokana na kutambua umuhimu wa kundi hilo maalum mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga amemuagiza kufikisha salamu hizo kwa kundi hilo maalum kwenye maeneo machache ya Ludewa ambayo aliona amefanikisha jambo juu yao.


"Tulianza kijiji cha Mavanga pale kulikuwa na mlemavu ambaye mbunge alimuona kipindi cha kampeni alikuwa na uhitaji wa msaada wa baiskeli hivyo kwa niaba yake tumemkabidhi baiskeli hiyo yenye thamani ya shilingi laki tano" Alisema Gowele.


Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Ludewa ambaye pia diwani wa kata ya Mundindi Wise Mgina wanafunzi hao wakipewa elimu inayofaa na wakapelekwa katika shule zinazostahili watakuwa na msaada mkubwa kwa jamii.


"Wanafunzi wanafaulu lakini wanapangiwa shule ambazo wakienda wanakutana na walimu ambao siyo wa elimu kada hiyo kuna changamoto kwa sisi wenyewe pengine hatufikishi ujembe kwa watu wakajua kama kuna mazingira Kama hayo" Alisema Wise.

Post a Comment

0 Comments