Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma imefanikiwa kurejesha Serikalini zaidi ya Milioni 11 ambazo zililipwa kwenye akaunti ya benki ya mtumishi marehemu kama mshahara kuanzia Oktoba 13, 2013 hadi March 2016 kinyume cha utaratibu.
Haya yameelezwa leo, December 1, na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma, Sostenes Kibwengo alipokuwa Akizungumza na Waandishi wa Habari.
Kibwengo amesema ufuatiliaji wa TAKUKURU Wilaya ya Kondoa umewezesha fedha hizo kupatikana.
0 Comments