Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amewataka Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na kuapishwa na Rais Dkt John Magufuli, kwenda kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu.
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Ikulu Chamwino jijini Dodoma baada ya Rais Magufuli kuwaapisha Mawaziri 21 na Naibu Mawaziri 22 aliowateua hivi karibuni.
Amewataka Viongozi hao kutolewa madaraka ya Uwaziri na badala yake wachape kazi ili waweze kuacha alama katika utumishi wao.
Spika Ndugai pia amewataka Mawaziri hao na Naibu Mawaziri kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Bunge ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanahudhuria vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge.
0 Comments