Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anapanga kuondoa amri ya kusitishwa shughuli za kiuchumi nchini humo kama ilivyopangwa Disemba 2, na kutangaza kurudishwa kwa vizuizi vya majimbo kufuatia kupungua kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Ofisi ya Waziri Mkuu huyo imesema serikali inapanga kurudisha tena mfumo wa vizuizi vya majimbo hasa kwa kutegemea kasi ya maambukizi katika eneo husika.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Johnson, baraza la mawaziri limepangwa kujadili mipango hiyo leo Jumapili huku Waziri Mkuu akitarajiwa kuliarifu bunge juu ya mipango hiyo mnamo siku ya Jumatatu.Serikali ya Uingereza ilitangaza amri ya kusitisha shughuli zote za kiuchumi kwa wiki nne kuanzia Novemba 5.
Vile vile, Ofisi hiyo imethibitisha mipango ya kuanza kutoa chanjo ya Covid-19 kuanzia mwezi ujao, lakini hilo litategemea iwapo chanjo hiyo itaidhinishwa rasmi.
0 Comments