Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe
imesema ipo mbioni kutengeneza utaratibu wa kuwabana na kuwachukulia hatua kali
za kisheria vijana wanaojiunga na mafunzo ya jeshi la akiba na kisha kushindwa
kumaliza mafunzo hayo kwa kutoroka ili hali tayari wameshafahamu mbinu za awali
za kijeshi.
Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauteri Kanoni
ameyasema hayo mbele ya hadhara ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba 166
wakiwemo wanawake 21 waliomaliza mafunzo kwenye Kata ya Makoga wilayani
Wanging’ombe mkoani humo ambapo amewaasa wahitimu kuwa wazalendo na nchi yao..
“Tutatengeneza utaratibu ukishajiandikisha na
ukishahudhuria mafunzo,ukapata ABCD za jeshi kidogo harafu ukatoroka
tutakukamata kama muarifu.Kwasababu tayari umepata siri za jeshi na sasa hivi
mnatambulika kama askari na kupitia kiapo chenu mmeapa kwamba mtailinda na
kuitumikia nchi hii kwa uadilifu mkubwa”alisema Lauteri Kanoni
Nao wahitimu wa mafunzo hayo akiwemo Josmo Mlwanda
wamesema katika mafunzo hayo wamekumbana na changamoto ikiwemo ikiwemo vijana
kuto tambua umuhimu wa mafunzo ya mgambo pamoja na upotoshaji kuwa mafunzo hayo
ni unyanyasaji
Aidha suala la uhaba wa Sare za jeshi la akiba
maarufu mgambo nalo limeonekana ni changamoto kubwa ambapo mshauri wa mgambo wilayani Wanging’ombe,
Kaptein Godwin Kimaro amesema baadhi ya wanafunzi wameshindwa kumudu ghalama za
mavazi huku mkuu wa wilaya hiyo akiagiza halmashauri kutenga bajeti kila mwaka
kwa ajili ya kununua mavazi hayo.
“Naielekeza
halmashauri kutenga bajeti kwa kila mwaka kwa ajili ya kununua mavazi ya askari
mgambo”aliagiza Kanoni
0 Comments