Na Amiri
Kilagalilia,Njombe
Mbunge wa viti maalumu mkoani Njombe Neema Mgaya amekabidhi
msaada wa taulo za kike 1600 zenye thamani ya shilingi milion 4
kwa wanafunzi wa kike katika za sekondari Maria Nyenyere,Makambako sekondari,Yakobi sekondari na Manyunyu sekondari. zitakazo weza kuwasaidia wanapokuwa hedhi.
Mara baada ya
kukabidhi taulo hizo amesema, ametoa taulo hizo baada ya kutambua changamoto
zinazowakabiliwa watoto wa kike pindi
wanapokuwa hedhi.
Mbunge huyo amesema wanafunzi wengi hasa wa kike
wamekuwa wakishindwa kusoma kwa bidii hasa wanapokuwa hedhi kutokana na kuathirika kisaikolojia kwa sababu
ya kukosa vifaa hivyo.
Afisa elimu taaluma halmashauri ya mji wa njombe
HURUMA CHAULA amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa
wakifanyiwa matukio ya ukatili wa kijinsia hasa
kupata ujauzito hasa wanapokuwa katika kipindi hicho kutokana na kutopata elimu na vifaa husika.
Mkuu wa shule ya sekondari Yakobi iliyopo wilayani
Njombe EDITHA HEDRICK JOHN amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao na kuwasaidia taulo hizo za kike
ili waweze kushiriki vipindi vyote wakiwa shuleni.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari yakobi wamesema
kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
ya kukosa baadhi ya vipindi shuleni hasa wanapokuwa
kwenye hedhi kutokana na kukosa taulo.
0 Comments