TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Zaidi ya wakulima 5200 wa zao la parachichi kunufaika na umeme jua



Na Amiri Kilagalila,Njombe 

Wakulima wapatao 5200 wa zao la parachichi mkoani Njombe wanatarajia kunufaika na zao hilo linalohitaji maji mengi  baada ya kuwa na  uhakika wa kupata maji ya kumwagilia kupitia umeme wa solar pump.

Hayo yamesemwa na wakulima wa parachichi mkoani Njombe baada ya kukopeshwa solar kutoka kampuni ya Ensol ambayo imekuwa ikiwafungia wakulima wa parachichi ili waweze kupata maji mengi ya kutosha kutoka kwenye visima ambapo awali walikuwa wanayakosa.

Miongoni mwa wakulima walionufaika na mradi huo wa kufungiwa solar akiwemo Paiasi Msigwa na lawino Msalilwa wamesema tangu wajiunge na Asasi ya wakulima wa parachichi mkoani Njombe (NSHIDA) inayowasaidia wakulima wa parachichi kupata pembejeo za kilimo cha hicho mwanga wa mafanikio umeanza kuonekana.



Wamesema kabla ya kufungiwa Solar wakulima hao walikuwa wanatumia kiasi kikubwa cha gharama katika kununua mafuta ya jenereta ili kuweza kuvuta maji kutoka kwenye visima hata hivyo maji yaliyokuwa yanapatikana yalikuwa hayakidhi mahitaji ya shamba zima.


"Nina imani kupitia haya maji sasa nitapata matunda bora kwani maua hayawezi kupukutika na hata matunda madogo pia hayawezi kupukutika kwakuwa dawa ya kwanza ya zao la Parachichi ni maji" Alisema Msigwa.

"Kabla ya kufungiwa solar hasara ambazo tulikuwa tunakutana nazo ni kuwa wakati tulipofikia kuvuna tulikuwa tunapata .atunda yasiyokuwa bora na kiwango kidogo yaani badala ya kupata kreti kumi za parachichi unapata kreti tano" Alisema Msalilwa.

Mkurugenzi wa NSHIDA Frank Msigwa amesema Asasi hiyo imekuwa ikiwasaidia wakulima wa parachichi katika uzalishaji na masoko lakini wamekuwa wakikumbana na changamoto nyingi ikiwemo.upatikanaji wa maji.

Alisema kupitia NSHIDA walitafuta fedha kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ambao ni wanachama wao wenye sifa ya moja kwa moja ya kukopesheka kupata miundo mbinu ya maji.



"Mkulima tuliyomtembelea amekopeshwa fedha anafungiwa miundo mbinu ya maji kupitia Solar pump hivyo ataanza kulipa kidogo kidogo wakati wa mavuno" Alisema Frank.

Mkandarasi wa kampuni ya Ensol inayoshughulika na ufungaji wa Solar pump kwa wakulima hao wa parachichi Julius Mwakalukwa alisema wamekuja kuwekeza kwa kuwasaidia  wakulima kutokana na shida wanazopata za kushindwa kuendesha kilimo cha umwagiliaji.

"Tumeona tulete huu mradi ili uwasaidie wakulima kupata mazao kwa kiwango kikubwa na kwa urahisi zaidi" Alisema Julius.

Mpaka sasa zaidi ya wakulima 100 wa zao la parachichi mkoani wamenufaika na mradi huo wa Solar pump utakaowawezesha kuvuna kiasi kikubwa na kilicho bora cha parachichi ambapo watauza kwa bei nzuri.

Post a Comment

0 Comments