Miili ya wahamiaji 8 waliozama kwa mashua kusini mwa Lanzarote wakati ilipokuwa ikiwasafirisha kutoka Kisiwa cha Canary barani Afrika kuelekea Uhispania imepatikana.
Kulingana na taarifa zilizotolewa na maafisa wa Timu ya Kukabiliana na Hali ya Dharura Lanzarote iliarifiwa kuwa mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji 36 hadi 37 ilizama karibu na pwani ya Orzola kaskazini mwa kisiwa hicho hapo jana nyakati za saa 19.30 jioni.
Timu ya waokoaji ilifanikiwa kuokoa wahamiaji 28 wakiwemo watoto 7 miongoni mwao. Hadi kufikia sasa miili 8 imepatikana huku mtu mwingine mmoja anayedhaniwa kuwa ndani ya boti hilo akiendelea kutafutwa.
Katika maelezo ya awali yaliyotolewa kwa polisi, wahamiaji walisema kuwa walianza msafara wao kutoka pwani ya Agadir nchini Morocco siku 3 zilizopita.
Wakati wa uchunguzi, timu ya waokoaji wa Uhispania pia walisaidia mashua nyingine ambayo ilisemekana kutoka Morocco na kusafirisha wahamiaji 19 ambao baadaye walipelekwa pwani.
Katika miezi miwili ya mwisho, idadi ya wahamiaji kutoka Afrika wanaosafiri kutoka kisiwa cha Canary imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kukaribia 18,000 wa mwaka huu.
0 Comments