Na Amiri Kikagalila Njombe
Mbunge wa Jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakili Msomi Joseph Kamonga ameendelea na mikutano ya kampeni za Kumuombea kura Rais Dkt John Pombe Magufuli na madiwani wa CCM ikiwa zimebaki Siku 16 kuelekea Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu nchini Tanzania hapo Oktoba 28, 2020.
Kamonga akiwa katika kata ya Madilu wilayani Ludewa amewashukuru Wananchi wa eneo hilo kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi na kumpitisha yeye bila kupingwa kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa na amewaahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri ikiwemo swala la Barabara.
''Ndugu zangu nimekuja kusema Asante sana,Jambo la pili nimekuja kuwaombea kura viongozi wa CCM, Tumekuja kumuombea kura Rais wetu Mpendwa Dkt,John Pombe Magufuli,tunamuombea kura Magufuli kwa ujasiri kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye taifa letu ni Rais wa kipekee mfano pekee mwaka jana aliweka utaratibu wa Kusikiliza Changamoto za wafanyabishara mbalimbali na aliweza kufuta kodi na tozo 114 zinazowaumiza wafanyabiashara na hii ni baada ya kubaini kuwa Zinarudisha nyuma maendeleo na mimi nitaiga mfano wa Rais Magufuli nitawasikiliza na kutatua cgangamoto zenu''. amesema Wakili Kamonga.
Aidha Mbunge huyo anayesubiri kuapishwa amesema changamoto Kubwa ya barabara ndani ya kata ya Madilu itapatiwa ufumbuzi chini ya viongozi wa CCM.
''Nafahamu kwamba barabara ya kutoka Lusitu kupitia Manga,Madilu , Ilininda hadi Mundindi ni Muhimu sana kwa afya ya Uchumi wetu wana Madilu, sisi ni wakulima wa Viazi na tunalisha Chipsi nchi hii,Tunazalisha Mbao,Chai,Ngano,Maharage na mazao mengine kwahiyo hii barabara ni muhimu sana hakuna sababu kwetu sisi kutokwenda kuipigania hata kama hawataweza rami basi ipitike wakatii wote ili kuinua Uchumu wa zaidi ya wakazi 9000 wa kata ya Madilu , tunajua Rais wetu mpendwa kwasasa yupo bize kuweka rami barabara inayounganisha Wilaya ya Ludewa na Wilaya ya Njombe kwa hiyo ndugu zangu tusimuache Rais Magufuli''.amesema wakili Kamonga.
Katika mkutano huo changamoto ya Umeme ikaibuliwa na wananchi wa kata hiyo ambapo waliwekawazi kuwa mgao wa umeme umekuwa mkali jambo ambalo linasababisha kushindwa kufanyika kwa wakati shughuli za uzalishaji ikiwemo viwanda vidogo vidogo lakini Mbunge aliyepita bila kupingwa akawatoa hofu na kuwapa ahadi ya kufanyia kazi swala hilo la umeme mara baada ya Kuapishwa na ikiwezekana vijiji vya kata hiyo viwekwe kwenye mpango wa umeme vijijini (REA) .
Mbunge huyo ameshafanya mikutano ya kampeni kwenye kata 13 ambazo ni Manda,Ruhuhu,Iwela,Masasi , Lwilo , Nkomang'ombe,Luana , Mawengi,Mlangali,Lupanga,Madope Lubonde na Madilu na anaendelea kutembelea Kata 13 Zilizosalia ambazo ni Lugarawa,Mavanga, Mundindi,Mkongobaki ,Ludende , Ludewa ,Milo,Ibumi,Lupingu , Lumbila , Kilondo, Makonde na Lifuma Wilayani Ludewa kumuombea kura Rais Dkt John Pombe Magufuli na Madiwani wa CCM.
0 Comments