Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe wakili Joseph Kamonga aliyepita bila kupingwa,amewaeleza wakazi wa Mfalasi kata ya Madilu wilayani Ludewa kuwa wana kila sababu ya kukichagua Chama hicho kwa mara nyingine kutokana na mambo makubwa yaliyofanywa wakati wa usimamizi wa serikali ya awamu ya tano.
"Chama cha mapinduzi ndicho Chama pekee,ambacho kina mfumo bora wa uongozi kutoka chini,na hata shughuri zinapofanyika panafahamika.Lakini wale wenzetu hawana hata ofisi kweli mpo tayari kuwachagua hao!"Joseph Kamonga
Amesema Ilani ya CCM imezingatia mahitaji yote kwa wanaludewa "Chama cha Mapinduzi kina Ilani ambayo ipo vizuri na imezingatia masilahi ya wananchi wote, ukiangalia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa wilaya ya Ludewa kuna mambo ya msingi yameingia humo"Joseph Kamonga
Ameongeza kuwa "Kwa haraka haraka kuna barabara inayoanzia Itoni hadi Manda ipo humo itakamilika kwa kiwango cha rami,Kwa kuonyesha ukweli wa Jambo hili Rais wetu mpendwa Dkt,John Pombe Magufuli ametoa jumla ya bilion 167 kwaajili ya ujenzi wa Km 50 Kwa kiwango vha Zege". Amesema Kamonga kwenye mkutano wa kampeni za kumuombea kura Rais na Madiwani wa CCM.
0 Comments