Na Amiri Kilagalila, Njombe
Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe,Joseph Kamonga aliyepita bila kupingwa amemtaka mgombea mwenza wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu kuwaomba radhi wana Ludewa kwa kusema uongo hadharani Kwenye mkutano wa kampeni.
Mbunge huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za Kumuombea kura Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kata ya Lupanga wilayani Ludewa.
Ameongeza kuwa mgombea huyo amesema wananchi wanadanganywa juu ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege inayoendelea kujengwa kutoka Lusitu hadi Mawengi alipofanya mkutano wake siku ya Jana katika kata ya Mlangali.
Kamonga amesema Rais Dk.John Magufuli amewekeza bilioni 167.5 katika barabara hiyo ya rami kiwango cha zege ili wana Ludewa waweze kupata maendeleo ,
''Nimeshangaa jana mwana mpotevu mmoja wa chama kile kingine na mgombea wa nafasi ya juu kabisa anawadanganya wananchi wa Mlangali,anasema mnadanganywa juu ya barabara,jamani unadanganywa kwa kitu unachokiona kwakweli anatakiwa akirudi tena Mlangali apige magoti aombe radhi.
Wananchi wa Ludewa wanajitambua hivyo hawawezi kudanganyika kwa vitu ambavyo wanaviona kwa macho! hivyo Chadema wajipange upya juu ya sera zao kwa Ludewa kwa hili wamefeli", Alisema Mbunge Kamonga.
Aidha Kamonga amesema Rais Dkt. Magufuli amefanya Maendeleo makubwa sana katika maeneo mbalimbali ikiwemo elimu bure ambapo ametoa zaidi ya bilioni.29, ujenzi wa vyumba vya Madarasa 36 kwa shilingi milioni 720, ujenzi wa Matundu ya vyoo 64 kwa zaidi ya shilingi milioni 72, Ujenzi wa Nyumba za walimu 30 kwa shilingi milioni 750, utengenezaji wa viti na Meza za Wanafunzi 205 uliotumia zaidi ya milioni 12.
''Lakini Pia Kwenye Sekta ya afya Rais Magufuli amefanikisha ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya 13 na kukarabatiwa hospitali 1 , vituo vya Afya 4 na Zahanati 9 kwa zaidi ya bilioni 3 ikiwemo ukarabati wa kituo cha afya Mlangali kwa milioni 500 na Manda kwa Milioni 400'' Alisema Mbunge Kamonga.
"Hivi kwa Fedha zote hizi ambazo Rais Magufuli amewaletea Wana-Ludewa kwa ajili ya Maendeleo unafikiri utawaambia nini wakakuelewa? ndugu zangu wana ludewa tusifanye makosa ",
Kamonga kwa kuwataka wananchi wa ludewa kumchagua Rais Dkt John Pombe Magufuli na Madiwani wa CCM.
Aidha mgombea mwenza Salum Mwalimu alipokuwa Mlangali jimbo la Ludewa alisema“Watakapokuja hapa Chama cha Mapinduzi waulizeni 1995 tulikuwa na Uchaguzi tukachagua CCM,2000,2005,2010,2015 tulikuja hapa kwenye Uchaguzi wakachaguliwa hata kwa kuiba kura barabara walijenga? Wameshindwa kwa miaka 25 wanataka tuwape miaka 5 wataiweza?”alisema Salum Mwalimu
Aliongeza kuwa“Chadema tunawaahidi,wilaya ya Ludewa na wilaya ya Njombe ni kipaumbele chetu kama Chama serikali itakayoongozwa na Rais Lissu kuhakikisha mradi huu wa barabara unakamilika haraka iwezekanavyo. Kwasababu barabara hii imekuwa mtaji wa kura zenu watu wa Ludewa” Salum Mwalimu
Vile vile aliongeza“Niwaambie wanaLudewa na CCM hapa wapo,barabara hii haitokamilika mpaka miaka mitano ijayo na mtaendelea kupigwa change la macho,barabara inatumika kwa ajili ya kuomba kura lakini wakipata kura hawaikamilishi”Alisema Salum Mwalimu
0 Comments