TANGAZA NASI

header ads

Ditopile awapa makavu wanaoleta ubaguzi wa Dini, amuombea kura JPM

 



Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile amefika katika kata ya Kingale wilayani Kondoa kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kondoa Mjini, Ally Makoa na Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Abushehe.


" " Hatujawahi kuona kiongozi wa kidini anatangaza hadharani kuunga mkono chama cha siasa, leo eti mtu anajiita sheikh anatangaza kuwa waislamu wanaiunga mkono Chadema ambacho kimechukua pesa za mabeberu ili kiunge mkono ushoga, hatuwezi kukubali kuona mtu mmoja anaharibu taswira ya Dini zetu, tumkemee na tumkatae kwa nguvu zote.


" Dk Magufuli amefanya mageuzi makubwa kwenye nishati ya umeme leo kila kijiji kina umeme nchini nzima na hapa kwenu pakiwemo, ameboresha sekta ya afya kwa kujenga zaidi ya vituo 480 vya afya na kata ya Kingale hapa mlipata, kwenye vijiji sita vya kata hii mmepata Zahanati mbili na niwaahidi nitakuja hapa tushirikiane tujenge Zahanati nyingine ya tatu," Amesema Ditopile.

Post a Comment

0 Comments