Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka wagombea wa nafasi za udiwani na ubunge kupitia chama hicho, washirikiane na viongozi wa chama kuanza mapema mchakato wa kuandaa mawakala wao, ili waapishwe na wasimamizi wa uchaguzi, kama sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavyoelekeza.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho Mhe.Tundu Lissu ametoa agizo hilo alipokuwa akiomba kura kupitia mikutano yake katika majimbo na Bahi na Kongwa mkoani Dodoma.
Mhe.Lissu ambaye amekamilisha kampeni zake katika majimbo matano ya mikoa ya Singida na Dodoma ameendelea kuwaomba Watanzania wampigie kura nyingi za ndiyo zitakazompa ushindi utakaomwezesha kuunda serikali itakayoongozwa na CHADEMA
0 Comments