Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Ludewa aliyepita bila kupingwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakili Joseph Kamonga , ameendelea na kampeni za kumuombea kura Rais Dkt,John Pombe Magufuli na Madiwani wa CCM zikiwa zimesalia siku 9 kufanyika uchaguzi mkuu nchini Tanzania.
Akiwa katika kata ya Nkomang'ombe wilayani Ludewa Kamonga amewataka wananchi wa eneo hilo kuwachagua Viongozi wa CCM ili waweze kuwaletea Maendeleo ya kweli kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na amemtaka Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia CHADEMA kuwa mzalendo kwa kumpigia kura Rais Magufuli.
"Kutokana na mambo makubwa ya kimaendeleo aliyoyafanya Ludewa na Nchi Nzima basi namuomba yule Mgombea wa kile Chama Kingine awe Mzalendo Kura yake ampigie Dkt John Pombe Magufuli , kila upande ukiuangalia unaona mambo makubwa aliyoyafanya magufuli , Ziwa Nyasa Kuna Meli Tatu , Barabara kutoka Itoni hadi Manda inajengwa kwa Rami Kiwango cha Zege''.amesema Wakili Kamonga
Aidha mbunge huyo mteule amewahakikishia kufanyia kazi kwa haraka madai ya wananchi wanaodai fidia kwenye mradi wa makaa ya mawe kwani wakati wa Uthaminishaji wa maeneo hayo alihusika.
''Naijua changamoto ya fidia kwakuwa nilishiriki kwenye kufanya Uthaminishaji,alipokuja mgombea mwenza tulimueleza na aliahidi kwamba jambo la fidia lipo kwenye hatua nzuri na mara baada ya uchaguzi litaanza kufanyiwa kazi , nawahakikishia hilo tutalifanyia kazi''.amesema Wakili Kamonga
Kwenye sekta ya elimu Rais Magufuli amefanya Mambo mengi ndani ya wilaya ya Ludewa ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa 36 vyenye thamani ya shilingi Milion 720, Ujenzi wa matundu ya vyoo 340 kwa thamani ya shilingi milion 272,ujenzi wa Nyumba za Walimu 32 zenye thamani ya shilingi milion 480, utengenezaji wa Madawati 6036 kwa zaidi ya shilingi milioni 211 katika kuhakikisha Miundombinu ya Elimu inaimarika.
0 Comments