Na Michael Ngilangwa,Njombe
Baadhi ya vijana mkoani Njombe wametaka serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutoa elimu
ya mpiga kura kwa wananchi ili washiriki kupiga kura Octoba 28 mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa na vijana mbalimbali mkoani Njombe na
kusema elimu ya uchaguzi inapaswa kuendelea kutolewa kila mahali iwe kwenye
mikutano ya wananchi na sehemu za ibada.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri amehimiza
wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga
kura ifikapo Octoba 28 mwaka huu
kwaajili ya kuwapata viongozi wa kuongoza
miaka mitano ijayo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa jukwaa la vijana Mkoa wa
Njombe bwana Lukha Mgaya amesema
wamekuwa wakishirikiana na serikali
kutoa elimu ya uchaguzi kwa vijana na kuhimiza vijana kujitokeza
kwa wingi kwenda kupiga kura.
Akizungumza kwa njia ya simu msimamizi wa uchaguzi mkoa
wa Njombe Herman Danda amesema serikali kwa kushirikiana na mashirika binafsi wanaendelea
kutoa elimu kwa wananchi ili wajitokeza kwenda kupiga kura ifikapo Octoba 28
mwaka huu.
0 Comments