Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baadhi ya wanawake mkoani Njombe wamesema wameshindwa
kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
kutokana na kuzuiliwa na baadhi ya waume
zao.
Wamesema nafasi ya
mwanamke kwenye uongozi zimeendelea kupigiwa kelele kwaajili ya kutetea haki zao lakini wamekuwa
wanahofia kuharibu ndoa na wengine wanazuiliwa na waume zao.
Nao baadhi ya wanaume mjini Njombe wamekili kutowaruhusu
wake zao kuwania nafasi za uongozi kwa
ngazi za ubunge na udiwani kwa kuhofia kuolewa na wanaume wengine na
kusababisha ndoa kuvunjika.
Viongozi wa vyama vya siasa mkoani Njombe wamesema kuwa wametoa nafasi nyingi kwa wanawake kushiriki
kuwania uongozi isipokuwa baadhi yao wamekuwa waoga kujitokeza.
Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Njombe Teresia Yomo
amesema,kwa sasa wanawake
wanaonesha ushiriki mkubwa
kuwania nafasi za uongozi na kwamba mwanamke akiwa kiongozi atatetea haki za
wanawake wenzao.
0 Comments