Na John Walter-Hydom, Mbulu
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema vyama vya Upinzani nchini haviwezi kuongoza nchi kwa sababu hawana sera.
Ameyasema hayo Leo septemba 30,2020 akizungumza na wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini katika mkutano wa Mgombea Mwenza Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kunadi Sera za Chama cha Mapinduzi katika viwanja Vya Haydom.
Sumaye amesema Chama alichotoka CHADEMA, ni Chama cha Uwana harakati na hakina sera zozote za kuwasaidia wananchi.
'CHADEMA wanafikiri kuwa nchi ya Tanzania bado ipo mikononi mwa Wakoloni, wanapiga kelele utafikiri bado tunatawaliwa' alisema Sumaye
'Nilienda kule lakini baada ya kugundua hawana chochote nikaamua kurejea nyumbani' alisisitiza Sumaye
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Manyara Simon Lulu amesema Chama hicho kinajiandaa kwa ushindi wa kishindo kwa sababu kimefanya maendeleo kwa wananchi.
Amemweleza Mgombea Mwenza kiti cha Urais Tanzania Samia Suluhu Hassan kwamba katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 28 mwaka huu, Upinzani mkoani hapo hawataambulia hata kiti cha Udiwani.
0 Comments