TANGAZA NASI

header ads

Sudan yatangaza hali ya dharura ya kiuchumi



 Sudan imetangaza hali ya dharura ya kiuchumi baada ya kushuka kwa kasi kwa sarafu ya nchi hiyo wiki iliyopita.

Waziri wa Fedha Hibe Muhammed Ali amesema katika mkutano na waandishi wa habari uliorushwa kwenye runinga ya serikali kwamba kile kilichotokea katika masoko ya fedha za kigeni ni hujuma za kimfumo na kwamba wametangaza hali ya dharura ya kiuchumi baada ya kushuka ghafla kwa safaru yao.

"Kinachofanyika sasa ni kuhujumu uchumi wa Sudan na kuifanya serikali ya mpito ishindwe kupumua." alisema waziri huyo.

Akisisitiza kuwa Sudan haitokubaliana na hali hiyo, Ali amebaini kuwa sheria zinazotungwa kulinda uchumi zitatekelezwa kwa kuungwa mkono na jeshi la pamoja linalojumuisha polisi, jeshi na ujasusi.

Waziri wa Sheria wa Sudan Nasreddin Abdulbari ametangaza kuwa adhabu ya wale wanaofanya biashara haramu ya fedha za kigeni imeongezwa kutoka mwaka mmoja hadi miaka 10.

Msemaji wa Serikali Faisal Mohammed Salih, ambaye anadai kuwa maadui wa mapinduzi wanatumia uchumi kama moja ya njia za kupambana na mapinduzi hayo, pia

"Tunaweza kusema kwamba kilichotokea katika siku chache zilizopita ilikuwa vita na hujuma za makusudi dhidi ya mapinduzi na serikali ya mapinduzi." alisema.

Post a Comment

0 Comments