Wizara ya maji na umwagiliaji nchini Tanzania
imeokoa zaidi ya bil 5 zilizokuwa hatarini kutafunwa katika mradi wa maji kata
ya Kinyika Tarafaya Matamba wilayani
Maketemkoani Njombe ambao umefikia
asilimia 98 na kughalimu shilingi milioni 900 huku mpaka kukamilika kwake
ukitarajia kugahalimu Bil 1.5 badala ya bil 6.7 zilizokuwa zimepangwa awali
kutumika.
Mafanikio hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa
maji Jumaa Aweso wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe ambapo amesema
serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi katika miradi inayotekelezwa na
wakandarasi na kuagiza mamlaka za maji kuanza kutumia Force Accountna wataalamu wa
serikali katika kutekeleza miradi hiyo.
“Mradi huu ulitaka kutekelezwa kwa Bil 6.7 sisi
baada ya kufanya ziara tukasema hapana,msituambie tu Bil.6.7 mkatuuzia mbuzi
kwenye gunia,kwasababu wizara ya maji imeajili wataalamu,tunakabidhi kazi hii
kwa wataalamu wetu badala ya kumpa mkandarasi na mradi mpaka sasa upo 98%
wametumia milioni 900”Alisema Aweso
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe
Ruth Msafiri amemueleza naibu waziri kuwa licha ya wizara kuendelea kupambana
na swala la maji lakini bado kuna vijiji na miji inakumbwa na uhaba wa huduma
ya maji.
“Hapa kuna changamot kubwa sana ya maji lakini
ukizungumza na mamlaka anakwambia mpaka aende Iringa na sisi kasi ya mji
inakuwa tunaomba sana tusaidiwe na kwamba mradi wa Hagafilo ukikamilika
tutapata maji nay a ziada”alisema Ruth Msafiri
Naye
kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Makete Injinia Innocent Lyamuya,amesema mradi
huo utakapokamilika utawafikia jumla ya wakazi 15,320 wa vijiji 9 vya tarafa ya
Matamba.
“Mradi
huu ukikamilika utahudumia vijiji vipatavyo tisa vya
Matamba,Kinyika,Mpangala,Ngonde,Mboje,Mbela,Mlondwe,Nungu pamoja na Ndapo.Eneo
la mradi huu lina jumla ya wakazi wapato 15,320 ambapo mpaka sasa wanaopata
huduma ya maji safi ni wakazi 13821 sawa na asilimia 90.2”alisema Lyamuya
Baadhi ya wananchi wa kata ya Kinyika akiwemo
Zedekia Mahali wanasema awali kata hiyo lkuwa ikikubwa na changamoto kubwa ya
ukosefu wa maji lakini kukamilika kwa mradi huo kumeongeza furaha kwao.
“Tunarudisha
shukrani kwa niaba ya wananchi wote wa kata ya Kinyika,maji tunayo ya kutosha
na nyumbani wananchi wana amani”alisema Zedekia Mahali
0 Comments