TANGAZA NASI

header ads

Watendaji idara ya ardhi wapewa maagizo Mkuranga



 MKUU wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Filberto Sanga amewataka wananchi wanaovamia mashamba ya watu katika Kijiji cha Vianzi kuacha mara moja kufanya hivyo kwani sheria itachukua mkondo wake.

Ameyasema hayo baada ya kwenda kutatua mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Vianzi na familia moja iliyonunua ekari zaidi ya 30 miaka mitatu iliyopita na wananchi waliopisha operesheni sogeza miaka ya 76 .

Amefafanua wapo baadhi ya wananchi wanaotoka mikoa tofauti nchini ambao wamevamia maeneo ya watu na kugawana huku wengine wakiuza kinyume na taratibu hali iliyoibua mgogoro uliokuwa ikitishia uvunjifu wa amani kwenye kijiji hicho.

Mkuu huyo wa Wilaya ya ametoa maamuzi ya Serikali baada ya kusikiliza pande zote mbili kati ya wananchi wenye mashamba yao yaliyovamiwa na wavamizi waliounda umoja wao wa wakulima huku akitoa maagizo kwa watendaji idara ya ardhi kulishughulikia suala hilo.

Pia ameagiza maeneo yote yaliyonunuliwa lakini hajaendelezwa yaorodheshwe ili yarudishwe serikalini na kuyatekeleza na kubakia mapori.

Aidha wote walioingia bila utaratibu katika mashamba ya watu waorodheshwe majina yao na wenye maeneo nao waorodheshwe ili mgogoro huo umalizwe kisheria kwa makubaliano.

"Kama kuna waliokubaliana itajulikana na kama kuna wavamizi itajulikana tu, kila mtu atapata haki yake hakunakitakachoshindikana,"amesema.

Amesisitiza utaratibu wote uanzie kijijini kwa makubaliano kati ya wenye maeneo na wavamizi kna ama kuna gharama upande mmoja utalazimika kulipia ifanyike hivyo.

"Isije kutokea kama ilivyotokea Magodani wananchi kuvamia ardhi kwa kutoelewa agizo la Rais Magufuli wanapigiana simu, wanagawana ardhi kama njugu hilo halitkubalika bali fuateni maelekezo nilitoyatoa kwani ardhi haiokotwi m ni vema kila upande upande haki stahiki,"amesema.

Amewashukuru wazee wa Vianzi kwa kukubali jambo liishe kwa kuzingatia sheria huku baadhi wakiomba Serikali iangalie usalama wao wakihofia vitisho kutoka kwa wavamizi hao.

"Kama waliingia kwenye mashamba ya watu kwa kununua imekula kwao lazima wenye ardhi zao wauze ama kugawa kwa makubaliano ai vinginevyo nje ya hapo wavamizi wote wataondolewa,"amesema,

Kuhusu hofu ya wazee kwa wavamizi kutishia amani kwenye maeneo yao amewahakikishia hakuna atakayethubutu kuvunja amani iliyopo kwani serikali iko makini.

Kero nyingine iliyojitokeza katika mkutano huo ni pamoja na wananchi kulalamikia mashamba yao kuvamiwa na wafugaji ambapo Mkuu wa Wilaya amewahakikishia hilo wanalifanyia kazi kwani changamoto kubwa iliyopo ni wafugaji kuishi maisha ya kuhamahama.

Amesema baadhi ya watendaji wa vijiji nao wamekuwa wakishiriki kuwaingiza wafugaji wengi kinyume na utaratibu kwa kupewa fedha kidogo ili wawalinde.

Post a Comment

0 Comments