Na Amiri Kilagalila,Njombe
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka
amewataka wataalam wa ujenzi wa barabara,madaraja na hata majengo kuacha
kufanyakazi kwa mazoea kwa kuwa mkuu mpya wa mkoa aliyeletwa ni mtaalamu wa
masuala hayo.
Ole Sendeka ametoa wito huo wakati akifanya
makabidhiano ya ofisi ya mkoa wa Njombe kwa mkuu mpya wa mkoa huo na kwamba
yeye alifanyakazi kwa kuuliza wataalamu kwenye mambo ya kitaalamu kama ya
ujenzi lakini sio mkuu wa mkoa wa sasa.
“Kwa hiyo mmeletewa Injinia,huyu hamtacheza naye iwe
bara bara za TARURA za TANROADS uwe ujenzi wa majengo yeyote huyu
hamtamdanganya”Alisema Ole Sendeka
Pamoja na mambo mengine Ole Sendeka amekabidhi hundi
ya zaidi ya shilingi Bilioni tano ambazo ni fedha zilizookolewa toka kwa watu
wachache waliofuja fedha za iliyokuwa benki ya wananchi Njombe Njocoba na vyama
vya ushirika.
“Hi ni hundi ya shilingi bilioni 5.397 ya fedha za
wananchi ambazo zimerejeshwa baada ya Rais Dkt,John Pombe Magufuli kwamba wakuu
wa miko na wakuu wa wilaya kuhakikisha wale wote waliochukuwa fedha za vyama
vya ushirika,vyama vya msingi na SACCOSS wanazirudisha,na leo namkabidhi mkuu
wa mkoa wa Njombe ili akaweka utaratibu wa kuzigawa fedha hizi”aliongeza
Sendeka
Awali katibu tawala mkoa wa Njombe Catalina Revocati
amesema kuwa Ole Sendeka enzi za utawala wake alikuwa kiongozi wa mfano kwa
kuwa aliweza kuwaongoza watendaji wake wote kwa kuzingatia maelekezo yake
anayoyatoa na kuyafanyia kazi kikamilifu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ofisi ya mkoa
mkuu mpya wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Mwita Rubirya amesema anatarajia
kuona viongozi wa ngazi za wilaya na halmashauri wanakuwa wa kwanza kutatua changamoto za wananchi
kabla hazijamfikia yeye kama kiongozi mkuu wa mkoa.
“Tuna wajibu mkubwa kuhakikisha tunasaidia wananchi
katika kutatua kero zao,mwananchi anaposhindwa kutatuliwa kero zake hakika
anasononeka,sasa nitashangaa kuona kuwa kuna kero ambazo zimetokea katika
wilaya Fulani mpaka anayelalamika aipeleke kwenye mamlaka za juu”alisema
Rubirya
Mhandisi Rubirya aliteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Njombe
mara baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo kwenda katika majukumu mengine ya
kisiasa

0 Comments