Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mtia nia wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia
na maendeleo Chadema ambaye pia ni mwenyekiti wa kanda ya kati Lazaro Nyalandu amesema chama
hicho kitaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba
mwaka huu kwakuwa kimetengeneza muunganiko mzuri baina ya mgombea Urais,Ubunge,Udiwani
na wananchi.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kufanyika kwa mdahalo wa kuwachuja watia nia wa nafasi ya
ubunge jimbo la Njombe mjini ambapo ametumia fursa hiyo pia kuomba udhamini kwa
wajumbe ili kupeperusha bendera ya nafasi ya Urais Nyalandu amesema kwa kuwa Chadema
kimezidi kufanya mambo yenye mvuto kwa umma wana imani kitaibuka kidedea katika
nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
“Kama unagombea Udiwani,Ubunge naomba ujiandae
kufanya kampeni tena ufanye kampeni kweli kweli kama unategemea utakuja
kutangazwa unapoteza muda wako hata tangazwa mtu atatangazwa mshindi”alisema
Nyalandu
“Ushauli wangu kwa wanaccm kama unadanganywa
umeshinda ubunge sijui udiwani umechukulia poa utatangazwa, mimi kama mwanaccm
wa zamani na ushauri wa bure wewe mwenzangu piga kampeni ya kufa mtu kwasababu
Chadema ya 2020 sio Chadema poa’aliongeza Nyalandu
Awali watia nia wakimwaga sera katika mdahalo huo
ulioongozwa na kauli mbiu ya "Njombe Tuitakayo" Akiwemo Sigrada
Mligo, Emmanuel Masonga na Rose Mayemba
wameweka bayana vipao mbele vyao endapo watapata ridhaa ya chama
kugombea.
“Chadema ndicho chama ambacho kina wabunge wenye
hoja thabiti na niwachache lakini wanapambana”Alisema Lusia Mlowe aliyekuwa
mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Njombe
Katika uchaguzi wa kura za maoni ushindani mkubwa
umekuwa kwa mgombea wa 2015 wa jimbo hilo Emmanuel Masonga na Rose Mayemba
lakini chaguo la wanachama likamwangukia Eammanuel Masonga ambaye ametoa shukrani kwa
wajumbe kumchagua kupeperusha bendera ya chama kwa nafasi ya ubunge katika
uchaguzi mkuu na kuahidi kutokiangusha chama hicho.
0 Comments