Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Balozi wa Indonesia
nchini Tanzania Profesa Ratlan Pardede amewatembelea wakulima wa
parachichi na kiwanda cha kuzalisha nguzo na mbao kupitia kampuni ya Tanwat
ambapo ameahidi kuimarisha mifumo ya biashara ya mazao hayo kwa kuanzisha
mikakati ya kuwa na biashara za moja kwa moja baina ya Tanzania na
Indonesia.
Amesema bei wanayouza
parachichi wakulima mkoani Njombe ni mara 6 huko nchini Indonesia hivyo
wakulima wamekuwa wakipoteza fedha nyingi kwa kupitisha mazao kwa madalali
ambapo ameahidi kuunganisha wafanyabiashara wa nchi zote mbili ili zao hilo
liwe na tija.
“Tutaweka karibu zaidi
wakulima wa parachichi Njombe na
ushirikiano wa watu wa Indonesia”alisema Pardede
Antery Kiwale ni
meneja mkuu wa misitu katika kampuni ya Tanwat amesema ujio wa balozi wa
Indonesia utasidia kuimarisha masoko ya bidhaa zinazozalishwa huku steven
mlimbilila mkulima wa parachichi akisema zao hilo linahitaji
usimamizi wa serikali katika kutafta masoko.
“Ujio wa balozi
hususani hapa TANWAT na Njombe ni fursa kubwa kujitanua zaidi hasa katika
upatikanaji wa masoko ya bidhaa za misitu na kwasasa tunayochangamoto kubwa ya
bidhaa zetu kwa mfano mbao”alisema Kiwale
Balozi Pardede pia
amefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa aina mbalimbali mjini Njombe wakiwemo
wachimbaji wadogo wa madini na kuahidi kuyaalika makampuni ya nchini kwake
kufanya biashara kwa ukaribu na wafanyabiashara wa mkoani hapa.
0 Comments