TANGAZA NASI

header ads

Museveni aruhusu bodaboda na texi kubeba abiria


Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameruhusu waendesha boda boda na texi kuwabeba abiria kwa masharti kwamba lazima wavae barakoa kuzingatia muongozi wa kuzua maambukizi ya corona.

Rais pia alipunguza muda wa kafyu kwa saa mbili - sasa itaanza saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.

Katika hutuba yake kwa taifa iliyorushwa moja kwa moja kwenye runinga usiku wa Jumanne, Bw. Museveni pia aliruhusu kufunguliwa kwa saluni na baadhi ya maduka makubwa yanazingatia viwango vya afya.

Vyombo vya habari nchini humo viraripoti kuwa maduka 110 syamefikia masharti yaliyowekwa.

Pikipiki zinazojulikana kama boda boda zitaruhusiwa kufanya kazi hadi saa kumi na mbili jioni kuanziaJulai 27.

Amesema mabadiliko hayo yamefikiwa kufuatia ushauri kutoka kwa wanasayansi.

Awali wahudumu wa boda boda waliruhusiwa kubeba bidhaa pekee yake kwa kuhofia itakua vigumu kwa abiria na muendeshaji piki piki kutukaribiana.

Waendeshaji boda boda waliishitaki serikali kwa kupiga marufuku biashara yao wakisema hatua hiyo imewaathiri kiuchumi.

Uganda kufikia sasa imethibitisha kuwa na watu 1,072 waliambukizwa virusi vya corona. Hakuna mtu yeyote aliyefariki kutokana na ugonjwa wa corona.

Post a Comment

0 Comments