Na John Walter-Babati
Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Manyara aliyemaliza muda wake Ester Alexander Mahawe ameibuka kidedea katika kura za maoni kugombea jimbo la Babati Mjini.
Ester Mahawe ameshinda kwa kupata kura 91.
Nafasi ya pili imeshikwa na Chambiri Werema kwa kupata kura 77 na nafasi ya tatu imekamatwa na Mbunge wa Babati mjini aliemaliza muda wake Paulina Gekul aliyepata kura 61.
Hakuna kura ziliharibika kwenye kinyang’anyiro hicho.
Jumla ya watia nia walikuwa 32 ambao wamejitokeza kwa jimbo hilo la Babati Mjini.
0 Comments