TANGAZA NASI

header ads

PARIMATCH YAJA NA MBINU HII KUSAIDIA JAMII


Na Mwandishi wetu

Kampuni ya Parimatch Tanzania  imetoa msaada wa chakula na nyenzo za kujifunzia kwa watoto wenye mahitaji muhimu  ili kuweza kuendana na kasi ya tecnolojia na kujiandaa vyema na mahitaji ya soko la ajira na kuweza kujiajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtandaji wa Kampuni hiyo, Tumaini Malinga amesema kuwa, wametoa kompyuta 10 kila kituo na runinga mbili lengo ni kuweza kuwaendeleza watoto hao katika masula ya elimu.

Amesema kuwa, kwa sasa wameanza na vituo viwili vya makao ambavyo ni huruma Islamic pamoja na Amani Foundation vilivyopo jijini Dar es Salaam, huku lengo ikiwa ni kuisaidia jamii katika masula mbalimbali ikiwemo elimu, mazingira pamoja na Michezo.

Kwa uapnde wake Balozi wa Kampuni hiyo  Diamond Platnumz amesema Parimatch iko katika misingi ya kusaidia jamii katika nchi zaidi ya 15 duniani huku misingi yake ikiwa ni kusaidia katika nyanja za elimu, Michezo na mazingira.

Aidha ameongeza  kuwa, Kampuni hiyo imeanzisha program inayoitwa AMSHA NDOTO  inayopatikana katika tovuti ya www.amshandoto.parimatch .co.tz ambapo vijana wenye timu mtaani wanaweza kujaza fomu online ili vifaa vitakavyotolewa kila mwezi kwa timu tano waweze kupata.

Naye, Mwenyekiti Makao ya watoto,  Dainarose Moyo ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada wa huo kwani walikua hawajawai kupata hivyo amewataka na wadau wengine kuiga mfano huo.

Post a Comment

0 Comments