Na Ignatio Charles,Ludewa
Zoezi la uchukuaji na urudishaji fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Ludewa Mkoani Njombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) limekamilika likiwa na wagombe waliochukua fomu hizo 26 na waliorudisha 25 huku mmoja akijitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari katibu wa chama hicho wilayani Ludewa mkoani Njombe Comred Bakari Mfaume amesema mgombea aliyejitoa ni Christopher Magogo ambaye ni mhadhiri wa Chuo cha Kodi kilichopo jijini Dar es salaam.
Mfaume amesema kuwa mgombea huyo amejitoa kwa sababu za msingi kwake ambapo amedai kuwa ameamua kujitoa kutokana na kuwa yeye ni mtumishi wa umma na ameona wamejitokeza wagombea wengi sana hivyo ameamua kuwaachia ili waendelee na mchakato na atakayepatikana anaamini kuwa ataleta maendeleo katika jimbo hilo.
Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo limeisha salama katika ngazi zote za kata na wilaya ambapo mpaka wanakamilisha zoezi hilo hawajapokea malalamiko yoyote .
Aidha waliokamilisha zoezi hilo la uchukuajo fomu ni Dk. Saimoni Ngatunga pamoja na Augustino Mwinuka ambao walijaza na kurudisha na kufikisha idadi ya wagombea 25.
Baadhi ya waliorudisha fomu ni pamoja na Dk. Primus Nkwera,Dr,Joseph Kamonga, Deogratius Nchimbi, Goodluck Mgaya, Barnaba Mhagama, Eng. Alfales Cengula, Dk. Evaristo Mtitu, Baraka Lucas, Mwl. Renatus Njelekela, Dk. Philipo Philikunjombe, Mwl. Herman Yanga, Deo Ngalawa, Dk. Neema Mturo, na Evaristo Mtitu.
Zoezi hilo la uchukuaji fomu limefungwa rasmi jana July 17 ,2020 na kuanza mchakato wa kumpata mgombea mmoja atakayekiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi oktoba mwaka 25 mwaka huu.
0 Comments