Na Amiri Kilagalila,Njombe
Madereva wa bodaboda mjini Njombe wametakiwa kuacha
tabia ya kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi Pamoja kuifanya kazi
hiyo kuwa rasmi kwa kupata elimu katika vyuo vinavyotambulika na serikali ili
kuepusha ajali zisizo za lazima.
Wito huo umetolewa na COPLO Marwa Kisyeri pamoja na
DTO Godlisen Ndosa kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wilaya
ya Njombe kwa niaba ya kamanda wa polisi
mkoa wa Njombe wakati wa kuhitinisha kampeni ya kukomesha ajali barabarani kata
ya Mjimwema iliyoratibiwa kwa ushirikiano na chuo cha ufundi cha Tagaste
kilichopo mjini hapa na kumbatana na zoezi la gawaji zawaji kwa dereva bora wa
piki piki aliyepatikana kupitia zoezi hilo.
“Tumeona wapate elimu ili tuone je zile ajali
zinazopatikana kila siku zinapungua au la,na hatutaki kusikia ajali kwasababu
zinarudisha nyuma maendeleo yetu”alisema Ndosa
Katika kampeni hiyo iliyodumu kwa muda wa mwezi
mmoja,mkuu wa chuo cha udereza na ufundi TAGASTE kilichopo mji mwema
halmashauri ya mji wa Njombe ELENEUS MGIMBA.Amewakumbusha madereva bodaboda
kufuata sheria za usalama barabarani Pamoja na kuhamasishwa kupata elimu ya
udereva
“Tukianza na hili kundi la bodaboda tumeona ajali
nyingi zinaonekana zinasababishwa na hawa boda boda,kwa hiyo sasa tunajitahidi
kutengeneza mazingira ya kuwafikia kwasababu kundi kubwa wanakuwa hawajapita
kwnye vyuo na kupata misingi ya udereva wao”alisema Eleneus Mgimba
Serikali ya mtaa wa Mjimwema kupitia kwa mwenyekiti
wa mtaa LEONARD ETEN MKUPI inasema mtaa huo baadhi ya Watoto wamepoteza Maisha
na wengine kupata ulemavu kutokana na ajali na kuwa elimu ndio njia pekee
itakayokomesha ajali.
“Naamini kwa mafunzo haya ajali zitapungua kwa kiasi
kikubwa sana,tumepoteza watoto wawili pale mji mwema shule ya msingi mmoja
amepata ulemavu lakini mwingine tumeshampoteza kwasababu ya kuendesha vyombo
hivi bila utaratibu,lakini kwa mafunzo haya naamini vijana watakuwa wamepata
mafunzo na kuepusha ajali”alisema Leonard Mkupi
Kwa niaba ya madereva wa Boda boda,mwenyekiti wa
usafirishaji kupitia vyombo hivyo Bwana Fredy Ndelwa amesema wapo tayari
kuendelea kutii kila wanachoelekezwa kwa kuwa usafiri huo ndio unaotumika kwa
kiasi kikubwa.
“Tunatabia ya kusikiliza nini tunambiwa na tupo
tayari kutii kwasababu usafiri wa boda boda unakubalika na unaingia mahali
popote pale kwa hiyo sisi tunapenda sana elimu”alisema Fredy Ndelwa
Washindi watatu katika zoezi la kumpata dereva bora
wa usafiri huo wa boda boda kata ya mji mwema wamekabidhiwa zawadi mbali mbali
ikiwemo kofia ngumu za kujikinga na majeraha kichwani inapotokea ajali
0 Comments