TANGAZA NASI

header ads

Mkurugenzi wa YONO AUCTION MART LTD achukuwa fomu ya ubunge viti maalum,Njombe




Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD ambao ni mawakala wa kukusanya kodi ya Serikali Scolastika  Cristian Kevela,kama kada wa Chama cha Mapinduzi amefika ofisi za chama hicho mkoa wa Njombe na kuchukuwa fomu ya ubunge viti maalumu mkoa wa Njombe.

Scolastika Kevela amesema ameona haja na nia kubwa ya kuwatumikia wananchi wa mkoa wa Njombe kwa kuwa muwakilishi wao kwa sasa hususana wanawake ili kufikia lengo na haja ya kutatua matatizo ya wanawake mkoani Njombe.

“Nimekuja Njombe  kutimiza wajibu wangu wa kikatiba kama kada wa Chama cha Mapinduzi,nami sasa kama kada nimechukuwa fomu ya ubunge viti maalum mkoa wa Njombe” alisema Scolastika  Cristian Kevela 
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya YONO AUCTION MART LTD.

Aidha kutokana na utaratibu wa chama hicho amesema hawezi kuzungumza mambo mengi mpaka utaratibu mwingine wa chama utakapofika.




Post a Comment

0 Comments