Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya
amemuagiza meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na
Iringa NFRA pamoja na mhandisi mkazi wa
TBA kumsimamia mkandarasi anaye jenga maghala mawili ya
kuhifadhi chakula mjini Makambako
na kutaka maghala hayo kukabidhiwa mapema mwezi Disemba mwaka huu.
Kusaya amechukua uamuazi huo baada ya
mkandarasi anaye jenga maghala hayo kusuasua kukamilisha ujenzi ambao mpaka
sasa ulitakiwa uwe umekamilika na kuanza kuhifadhi nafaka mbalimbali
jambo ambalo limekuwa kinyume na makubaliano ya mkataba.
“Chukueni hatua TBA
tunachotaka ikifika disemba 31 mimi nije hapa tarehe moja mwaka 2021 mnikabidhi
majengo yangu hicho ndicho tunachotaka”alisema Kusaya
Awali kaimu meneja wakala wa taifa wa hifadhi
ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA Frank Felix amesema mpaka sasa kanda
hiyo yenye mikoa miwili ina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 22 na kuongeza
kuwa ukasanyaji nafaka utaongezeka mara baada ya maghala mawili yanayo suasua kujengwa
yakikamilika.
“Tumepangiwa jumla ya kununua tani elfu 30,ndani ya tani hizo tani elfu
tano tutanunua mpunga na elfu 25 tutanunua mahindi,lakini maghala haya mawili yatakuwa
na uwezo wa kuchukuwa tani elfu kumi kumi kwa hiyo jumla sasa ya mradi huu ni
tani elfu 40”alisema Frank Felix
Akizungumzia
changamoto za mradi wa ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhi nafaka mhandisi mkazi wa TBA Eng.Pedon
Mushobozi anasema uzembae wa mkandarasi,hali ya hewa pamoja na kusuasua kwa
malipo,yamepelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
“Changamoto kubwa hapa ni malipo
kwa mkandarasi na imepelekea mkandarasi
kuishiwa fedha”alisema Eng.Pedon Mushobozi
Katika hatua nyingine
katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amewataka wafanya kazi wote wanao
fanya kazi chini ya wizara yake kujiendeleza kielimu kwani kufanya hivyo
kunaongeza ufanisi kazini.
0 Comments