Na Jackline Kuwanda, DODOMA
Halmashauri ya jiji la
Dodoma imesema kuwa itahakikisha kuwa Dodoma inakuwa ya kijani huku ikipiga
marufuku ukataji wa miti na atakayetaka kukata miti kwa sababu yeyote ile ni
lazima apate kibali kutoka kwa Ofisi ya mkurugenzi wa Jiji.
Halmashauri pia imetoa
wito kwa wale wote waliopanda miti kuhakikisha wanaitunza vizuri miti hiyo.
Kauli hiyo imetolewa
na mkuu wa Idara ya mazingira na udhibiti wa taka ngumu katika halmashauri ya
jiji la Dodoma bwana Dickson Kmaro wakati akizungumza na Mtandao wa Dodoma News
Blog.
Amesema moja ya
majukumu waliyonayo pamoja na majukumu mengine ya udhibiti wa taka ngumu
,upendezeshaji miji, wanajukumu jingine la uhifadhi na utunzaji wa mazingira
kwani katika eneo hilo jukumu ambalo wanaendelea nalo kwa kushirikiana na
wadau mbalimbali ni suala zima la kukijanisha Dodoma ambayo ni kampeni
iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mh Samiah Hassan kaitka eneo la mzakwe.
Dkt Liberatus Domic
Lyimo ambaye ni mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Dodoma UDOM amesema tangu
walipoletewa miti walianzisha kampeni ya upandaji miti na vilevile wanaklabu za
wanafunzi za mazingira .
Mrakibu wa gereza
la Msalato Hamisi Nyaku amesema suala la kutunza mazingira katika Gereza
lao wamelipa kipaumbele kwa kiasi kikubwa .
Halmashauri ya Jiji la
Dodoma ipo makinikatika kutekeleza mikakati mbalimai ya kitaifa ya utunzaji na
uhifadhi wa mazingira ikiwemo mkakati wa kuhifadhi ardhi na vyanzo vya maji
Viongozi wa ngazi
mbalimbali wamekuwa msitari wa mbele katika kuhamasisha utekelezaji
wa zoezi hilo akiwemo Mhe. Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu
aliyezindua kampeni ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani mnamo tarehe 21/12/2017
ambapo ilipandwa jumla ya miti 2,300 katika chanzo cha maji Mzakwe ambayo
ilitolewa na TFS.
0 Comments