Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Balozi wa Indonesia
nchini Tanzania Balozi ,Professa dr
Ratra Pardede amesema kuwa atashauriana na wawekezaji wa nchini kwake juu
kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani Njombe kufuatia mkoa huo kuwa na
fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo uzalishaji mbao ufugaji na kilimo cha
parachichi na chai.
Akiwa mkoani Njombe Balozi professa dr
Ratra pardede ametembelea uwekezaji katika kiwanda cha chai cha kabambe
factory Pamoja na kiwanda cha kukamua parachichi kilichopo wilayani
wangingo’mbe.
“Baada ya kutembelea baadhi ya wawekezaji wa viwanda hapa
Mkoani njombe naamini kutakuwa na ushirikiano baina ya wafanyabishara na
wawekezaji kutoka nchini Indonesia na Njombe katika kuuziana mazao
mbalimbali baina ya nchi hizi mbili”alisema Balozi Ratra pardede mara baada ya kutembelea kiwanda
cha usindikaji na uchakataji wa
parachichi cha Olivado
Baadhi ya wawekezaji
mkoani Njombe wamesema kuwa ujio wa balozi huyo utasaidia ukuaji wa sekta hiyo
hasa katika kubadilishana teklojia Pamoja na kupanua Nyanja ya masoko .
“Kwanza tunashukuru
kwa ugeni uliofika katika kiwanda chetu cha Olivado tumepata hamasa kubwa
sana,ushirikiano ukiwpo mzuri utatusaidia kwenye maswala kwanza ya miundombinu
ikiwa ni pamoja na vifaa au mashine zinazotumika katika uzalishaji wa mafuta”alisema
Bosco moja wa kiongozi katika kiwanda cha Olivado
Katarina Revocat ni katibu tawala mkoa wa Njombe amezungumzia
ziara ya balozi huyo.
“Tutaweza kuiga njia
walizotumia wao hadi kufika pale walipofika,kwa hiyo huu ni wito kwa wananjombe
kuangali fursa kama hii ya namna ambavyo
tunaweza kushirikiana na Indonesia ili tuweze kupata kupanua masoko ya bidhaa
zetu”alisema Katarina Revocati.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania
Balozi ,Professa dr Ratra Pardede akitembelea na kujionea uwekezaji na uzalishaji wa majani ya chai
unaofanywa na kiwanda cha Kabambe Tea Factory kilichopo Lwangu halmashauri ya
mji wa Njombe.
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Balozi ,Professa dr Ratra Pardede akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha kuhifadhi na kuzalisha parachichi cha Tanzanice kilichopo mjini Njombe.
0 Comments