TANGAZA NASI

header ads

Aliyefanya mtihani wa Sekondari mara 17 hatimaye ahitimu


Kijana Emmanuel Oluwasayomi Ahmadu kijana kutoka Nigeria aliyehitimu chuo kikuu, ameonyesha kuwa mtu yoyote anaweza kufanya kitu kikubwa katika maisha yake, bila kujali changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.
Kabla ya kujiunga na mafunzo ya mwaka mmoja jeshini, Emmanuel alifanya mtihani wa kuhitimu sekondari mara 17, na mtihani wa kuingia chuo kikuu mara tano.
Katika mahojiano, kijana huyo amesema awali alikuwa na mtazamo hasi juu ya maisha yake, wakati alipowaona wenzake wakiendelea mbele na kuhitimu vyuo vikuu.
Lakini na kwake pia limetimia kwani mwaka huu, Emmanuel amemaliza mafunzo ya lazima ya mwaka mmoja jeshini baada ya kuhitimu chuo kikuu, huku akiwa na tuzo kadhaa.

Post a Comment

0 Comments