TANGAZA NASI

header ads

Wagombea 15 wa Udiwani viti Maalum tarafa za wilaya ya Njombe wapatikana



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Jumla ya wajumbe 493 kutoka tarafa nne za wilaya ya Njombe wamekusanyika (jana) ukumbi wa Turbo mjini Njombe kwa ajili ya kuwachagua madiwani wa viti maalumu kupitia uiya ya umoja wa wanawake wa UWT watakao wawakilisha kwa miaka mitano ambapo kila Tarafa wanahitajika madiwani viti maalumu watano.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe Bw.Edward mgaya aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuchagua viongozi ambao hawajihusishi na Rushwa kwani kufanya hivyo watapata viongozi waadilifu huku katibu wa UWT Mkoa wa Njombne Bi.Mary mkoka akisema kiongozi bora hapatikani kwa njia ya Rushwa.

"Acheni tabia hiyo mnakidhoofisha Chama,nawombeni sana wajumbe chagueni watu makini watakaojielekeza kusimamia Ilani na sio mambo mengine" alisema Edward Mgaya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe

Kila Mgombea  kwa Nafasi yake aliweza kujinadi ili kupata kura ya mjumbe kwa lengo la  kuwatumikia wananachi endapo atapewa ridhaa huku wengi wa wajumbe hao sera zao ni miundombinu,afya na elimu na wenginge wakiweka viapau mbele vyao binafsi.

Aidha Katibu wa UWT Mkoa wa Njombe Mary mkoka amewataka wapiga kura kuto kosea kupiga kura kwa viongozi sahihi  kwani wakikosea kuchagua sasa wakumbuke kuwa watataabika kwa miaka mingine mitano.

"Hawa watu mnakaa niny msikosee,wanenda kufanya kazi na ninyi kwa mika mitano tafuteni kiongozi ambaye hataki uongozi huu kwa ajili ya kujinufaisha yeye na familia yake"alisema Mkoka

Katika zoezi la upigaji kura za maoni kuwapata Madiwani viti maalumu tarafa zilizopo Wilaya ya Njombe matokeo kwa walioongoza kura za maoni zilikuwa kama ifuatavyo.

WAJUMBE=493
WAGOMBEA JUMLA=69

Tarafa ya Njombe mjini

-Njombe mjini ; Wagombea15

Tarafa ya Igominyi

-Igominyi  ;Wagombea  8

Tarafa ya Makambako

-Makambako ; Wagombea18

Tarafa ya Lupembe

-Lupembe ; Wagombea 28
 
MATOKEO YA KURA ZA MAONI

TARAFA YA NJOMBE MJINI

1.Angela Mwageni 384
2.Tumaini Jackson Mtewa 250

TARAFA YA IGOMINYI

1.Mariam Chundu 299
2.Catherine Simon 254
3.Koletha Pankras Nyigu 248

TARAFA YA MAKAMBAKO

1.Angelina Kimbawala 391
2.Stela Mhema 312
3.Flora Nyaluke 287
4.Lucy Mbogela 226
5.Apia Kalinga 204

TARAFA YA LUPEMBE

1.Neema Solomon Mbanga 284
2.Getruda Chungwa 230
3.Roida Wanderage 197
4.Faraja Mbanga 185
5.Daina Mangula 153

Post a Comment

0 Comments