“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo,kwa sasa wengi wanataka uwanja uitwe ‘Mkapa Stadium’, Mzee Mkapa alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini kwakuwa hawezi kuniadhibu chochote amelala hapo, natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium”-JPM
"Hata kwenye Michezo alitoa mchango tena nasikia alikuwa mshabiki mkubwa wa Yanga, ingawa sikuwahi kumsikia akisema hilo hadharani, Mzee
hapa ansema ni kweli kwa sababu na yeye ni Yanga, sifahamu Mzee Mwinyi yeye ni timu gani" - Rais
"Mtakumbuka wakati wa Mzee Mkapa ndipo kodi ya kichwa ilifutwa, kwa waliokuwepo kodi hii ilikuwa inasababisha matatizo makubwa kwa wananchi, alifuta kodi ya Baiskeli ambayo nayo ilikuwa ikisababisha matatizo pamoja na kodi ya mifugo nayo aliifuta" - Rais
"Watanzania wanamkumbuka Mzee Mkapa kwa mageuzi ya uchumi, wakati anaingia madarakani nchi yetu ilikuwa na matatizo ya kiuchumi, na wakati huo alianza kulipa madeni na kuanza kuzishawishi Taasisi za Kifedha pamoja na nchi wahisani kufuta madeni yake" -



0 Comments