Na Muhadh Mohammed, Songea Ruvuma. Mkazi wa kitongoji cha tanki la maji kata ya mkako wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma amejiuwa kwa kujipiga risasi baada ya kuwa na msongo wa mawazo wa kujaribu kum'baka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka kumi (10).
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Simon Marwa Maigwa amesema tukio hilo limetokea katika kitongoji cha tanki la maji kata ya mkako wilayani Mbinga mkoani Ruvuma amemtaja marehem Basilius Mwingira ambae alikutwa amejiuwa kwa kujipiga risasi shambani Kwake.
Aidha kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi litaendelea kufanya msako mkali kwa watu wote wanaofanya vitendo vya upigaji lamri chonganishi .
0 Comments