TANGAZA NASI

header ads

Wasio lipia ghalama za umiliki wa ardhi Njombe wapewa siku 90




Na Amiri Kilagalila,Njombe

Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Angelina Mabula ametoa siku 90 kwa wamiliki wa viwanja 31,270 mkoani Njombe ambavyo vimeshapimwa, kufika katika ofisi ya ardhi ili kulipia gharama za hati za umiliki wa maeneo yao vinginevyo watalazimika kulipishwa faini ya kipindi chote walichokuwa wamekamilisha upimaji bila kulipia.

Akizungumza wakati akizindua ofisi ya ardhi ya mkoa wa Njombe Mabula amesema kati ya 42,516 vilivyopimwa katika mkoa huo viwanja 11246 ndiyo vimelipiwa hati jambo ambalo linakwamisha mipango ya serikali kwa kutolipa kodi na kuagiza kwamba ifikapo julai mosi wamiliki wa viwanja zaidi 31 elfu wanapaswa kuanza kulipia ili wakabidhiwe hati zao vinginevyo watapigwa penati ya kulipa kodi kwa kipindi chote ambacho walikuwa wamepima bila kulipa.

“Kuanzia tarehe moja mwezi wa saba hawa wote thelathini na moja elfu mia mbili sabini muwatafute waliko wapeni envoice zao waje kulipia maeneo yao waje wapate hati zao”alisema Mabula

Kasi ya ukuaji wa Mkoa wa Njombe kiuchumi na idadi ya watu imezidi kukua kila uchwao tangu kuanzishwa kwake 2012 hatua ambayo inatajwa na kamishna wa ardhi mkoa wa Njombe Christopher Mwamasage kuwa ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi huku mkuu wa mkoa huo Christoper Ole Sendeka akisema kuanzishwa kwa ofisi hiyo kutapunguza usumbufu wa kufata huduma hizo mkoani Mbeya

“ Kutokana na hiyo kumekuwepo na migogoro ya mi[aka ya kimikoa,wilaya,vijiji na ardhi binafsi,mkoa umeshughulikia migogoro katika hatua mbali mbali na mingine imeshughulikiwa kiutawala na mingine kisheria”alisema Christopher Mwamasage

Baadhi ya wananchi walioshiriki katika uzinduzi huo na kukabidhiwa hati za viwanja na naibu waziri akiwemo Raurent Nikson ,Naomi Msafiri na Richard Mkalawa wanasema mkoa wa njombe umekuwa na mrundikano wa migogoro ya ardhi na kusababisha mrundikano wa mashauri kutokana na kukosekana na ofisi hizo hivyo ujio wake utakuwa na matokeo chanya .



Post a Comment

0 Comments