Na Amkiri
kilagalila,Njombe
Mwenyekiti wa umoja
vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Theopister Mhagama ametoa
rai kwa vijana wa chama hicho,kubadili mfumo wa siasa na kuacha siasa za fujo
na matusi badala yake kufanya siasa zenye ustaarabu na wenye kuruhusu
demokrasia.
Mhagama ametoa ushauri huo wakati akizungumzia mtazamo wao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu hasa kwa vijana.
“Tunataka vijana
kubadili mfumo wa siasa,tusifanye siasa za matusi na vijana wetu hatuwaruhusu
kufanya hivyo,tuliona hata kwenye chaguzi za serikali za mitaa siasa zilizofanyika
zilikuwa za kistaarabu mtu akishindwa anakubali ameshindwa na sio kufanya fujo”alisema
Theopista Mhagama
Vile vile amewashauri
vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM kujitokeza kwa wingi ili kuchukua fomu za kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama chao
“Kwa hiyo rai yangu
kwa vijana jinsi walivyohamasika katika uchaguzi wa serikali za mitaa,naomba
wajitokeze vile vile kwenye uchaguzi huu wa mwaka 2020”aliongeza Theopista
Aidha Bi, Theopister
ameongeza kuwa vijana wanatakiwa kuachana na nidhamu ya woga kwa kile
kinachodaiwa vijana wanakurupuka badala yake amewataka wajiamini kwa kuwa wanao
uwezo mkubwa.
0 Comments