Salvatory Ntandu
Wananchi zaidi ya 100 waliokumbwa na maafa ya kubomolewa kwa nyumba zao kutokana na mafuriko katika kata Ngaya,Bulige na Kashishi katika Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama mkoani Shinyanga wameomba kupatiwa elimu ya ujenzi wa makazi bora ili kuwawezesha kujenga nyumba za kisasa.
Wakizungumza katika hafla maalumu ya kukabidhiwa
misaada ya Magodoro,chandarua,blanketi na ndoo za maji yaliyotolewa na Shirika
la Msalaba Mwekundu iliyofanyika June 4 Mwaka huu katika kata za Ngaya na
Bulige iliyoongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha.
Merry Shija ni mmoja wa wahanga wa mafuriko hayo
alisema kuwa endapo serikali ikiwapatia elimu hiyo itawasaidia wao kujenga
nyumba za kisasa ambazo hazitapata athari zitokanazo na mafuriko pindi
yanapotokea hususani katika maeneo ya vijijini.
“Mwaka huu sisi tumevuna mazao ya
kutosha,tunatarajia kuanza ujenzi wa nyumba zetu zilizobomolewa na mafuriko
yaliyosababishwa na mvua za masika ambazo mwaka huu zimenyesha kwa
wingi,tutahakikisha tunatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa nyumba zetu,”alisema
Shija.
Nae Felista Bula alisema kuwa ukosefu wa elimu
ya ujenzi hususani vijijni bado ni tatizo kutokana na wengi wao kutokuwa na
maarifa ya ujenzi wa nyumba za kisasa hivyo ni budi serikali ikaona umuhimu wa
kutoa elimu ya ujenzi kwa wananchi.
Kwa upande wake meneja wa maafa nchini kutoka
shirika la msalaba mwekundu Simon Kadogosa alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu
ya mchango wao kwa jamii ili kuiunga mkono serikali hususani maafa yanapotokea
na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuhakikisha wanazingatia maelekezo ya
serikali kuhusiana na ujenzi wa makazi bora.
“Misaada hii imegharimu zaidi ya shilingi milioni 40
ambayo ni ndoo za maji,vyandarua,mashuka(Blanket) na Magodoro ambayo
yamegawiwa kwa wakazi zaidi ya 100 waliopata maafa hayo,”alisema Kadogosa.
Akitolea ufafanuzi suala hilo Mkuu wa wilaya ya
Kahama Anamringi Macha aliwataka wakazi hao kuhama mabondeni pamoja na maeneo
yenye mikondo ya Maji ili kuondokana na tatizo hilo ambalo limekuwa
likisababisha wanachi kuhangaika hususani kipindi cha Mvua zinapoanza kunyesha.
“Jengeni makazi bora kwa kutumia tofali za kuchoma
tumieni pumba za mpunga kuchomea tofali zenu ili muweze kuondokana natatizo
hilo ambalo linaweza kuzuilika sambamaba kujenga katika maeneo ambayo ni
salama yaliyotengwa kwaajili ya shughuli za Mkazi.


0 Comments