Mstaafu huyo ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa CCM wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne, alitangaza hadharani jana huko jijini Arusha kuomba msamaha kwa makosa aliyoyatenda kipindi chake cha uongozi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Arusha Kinana alisema akiwa
kiongozi anaamini kuwa yapo mambo aliyoyafanya ambayo yaliwakwaza
viongozi wengine akiwamo Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli, ambaye ni
Rais wa Tanzania na anaamini atamsamehe.
“Naamini
ilifika wakati nikakereka na kusema maneno ambayo yanaweza kuwa siyo
mazuri, nimekaa na kutafakari sasa, namuomba radhi Mwenyekiti wa CCM,
Magufuli,” alisema Kinana na kuongeza:
“Kama
kiongozi ni kweli naamini ilifikia hatua nikatofautiana na wenzangu ama
niliwakera wenzangu na pia, hata kiongozi wangu, Mwenyekiti wa Chama,
kiukweli ninamwomba radhi”na akaongeza kwa kusema kuwa mimi kwa sasa
nimestaafu uongozi,ninamshukuru Mungu na ninaendelea kujifunza,kusoma
vitabu na kufanya mazoezi na niko tayari lkuendelea na mchango wangu wa
hali na mali ndani na nje ya chama alisema.
Desemba
13, mwaka jana, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), iliagiza makada
watatu wa chama hicho akiwamo Kinana, waitwe na wahojiwe na Kamati ya
Maadili na Usalama, baada ya kutuhumiwa kwa makosa ya kufanya mambo
kinyume na taratibu za chama.
Kamati
Kuu, iliwaadhibu viongozi hao na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Memba, kufukuzwa uanachama kwa kukiuka
maadili ya chama hicho.
Hali Kadhalika,
Makamba alisamehewa huku Kinana akipewa barua ya onyo ikiwamo kuwa
chini ya uangalizi kwa miezi 18 na kuzuiliwa kujihusisha kugombea nafasi
yoyote ndani ya chama hicho.

0 Comments