Na Omary Mngindo, Bagamoyo
KATIKA mpango wa kunusuru kaya masikini hapa nchini na kuziongezea kipato, Tasaf kupitia utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu, inataraji kuzifikia kaya zaidi ya milioni 1. 4 kati ya milioni 7 nchini kote.
Hatua hiyo ikiwa ni nyongeza ya kaya laki tatu na nusu zaidi ya kipindi kilichopita, mkazo mkubwa katika kipindi cha pili umeelekezwa katika kuwezesha kaya zitakazoandikishwa kwenye mpango utaolenga kufanyakazi ili kuongeza kipato.
Hayo yamo katika tarifa ya ufunguzi wa mafunzo ya kikao kazi kwa cha Wakuu wa Idara na mafunzo kwa wawezeshaji wa Halmashauri ya Bagamoyo, iliyosomwa na Amadeus Mbuta Afisa kutoka Tasaf, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Ladislaus Mwamanga.
Imeeleza kuwa mpango huo unaolenga kutatekelezwa katika wilaya zote 185 za Tanzania Bara na Zanzibar, utekelezaji wake utaofanyika kwenye Vijiji, Mitaa, Vitongoji, huku upande wa Tanzania Visiwani ikijulikana kwa Shehia itajumuisha maeneo ya Vijiji ambavyo havikupata fursa hiyo.
"Wakati wa uzinduzi wa kipindi hiki cha pili, rais Dkt. John Magufuli aliagiza kwamba kabla ya shughuli zozote kuanza, uhakiki wa walengwa ufanyike nchini kote ili kuondoa kaya za walengwa ambazo zimepoteza sifa," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Imeongeza kuwa utekelezaji wa agizo la rais la kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii ya kuwemo walengwa hewa, Tasaf imetakiwa kuanza utekelezaji kwa kusafisha daftari la walengwa, kupitia mafunzo yanayolenga kujenga uelewa wa mpango huo na kuboresha kaya husika.
"Msingi wa kwanza lazima kila kaya ifanyekazi, Kijiji kiandae mpangokazi sanjali kuwepo lasirimali watu, hususani watoto ili kuleta matokeo chanya yatayodumu kwa muda mrefu, ikiwemo kuboresha upatikanaji wa huduma za maji, afya na elimu, hatua itayoongeza kaya kuongeza kipato," ilieleza taarifa hiyo.
Imefafanua kuwa wanatakiwa kuwepo orodha ya walengwa kwenye Masjala ya kaya husika, na kutambua waliofariki, waliohama, ikiwemo walioshindwa kuchukua malipo kwa mara mbili mfululizo kwenyepango uliopita, kaya ambazo zinahusika kuondolewa katika mpango huo.
Akitoa mada kwa wajumbe hao Shaaban Abdulmali Afisa Miradi alisema kuwa, katika mpango huo unatakiwa kuzihusisha Kamati za manunuzi kwenye maeneo husika, ili kwa upande huo uwakilishe vizuri jamii kuhusiana, kuhusiana na miradi na utekelezaji wake.
"Tunapokwenda kulitekeleza zoezi ili tuhakikishe kwamba viongozi wetu wanatoa taarifa zenye ukweli,ikiwemo waliofariki, kuhama na waliopoteza sifa kwani kinyume chake litakapoharibika kila mmoja atahusika katika eneo lake," alisema Abdulmalik.
Aidha alisema kuwa mpango huo kwa Halmashauri ya Bagamoyo wawezeshaji 26 watasimamia zoezi hilo, ambapo wanataraji kuwafikia walengwa wa 3,131wanaotaraji kunufaika na utaratibu huo, huku akiwapa taadhali wakati wa kilifanyiakazi zoezi hilo.
Awali akizungumza na wakuu wa Idara pamoja na wawezeshaji, Dionis Mahilane Mratibu Tasaf Bagamoyo aliwaambia Wakuu wa Idara kuwa kufika kwao kwenye kikao hicho unalenga kuwajulisha uwepo wa zoezi hilo, na kwamba kwa Bagamoyo baadhi ya watumishi wao wanasimamia mpango huo.
0 Comments