TANGAZA NASI

header ads

Tanzania kuendelea kutafuta masoko ya uhakika ya minofu ya Samaki


Dodoma.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ameongoza kikao kazi cha kutathmini namna nzuri ya kusafirisha minofu ya samaki nje ya nchi kilichokutanisha Wizara ya fedha,Wizara ya Mifugo na Uvuvi , Wizara ya kilimo Pamoja na wakuu wa mikoa ya Mwanza,Kagera na Mara.
Akizungumza   na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Mara baada  kuhitimisha kikao  hicho Mhandisi Kamwelwe amesema lengo la kikao kazi hicho ni kutafuta masoko ya uhakika ambapo amesema tangu Tanzania ianze kusafirisha minofu ya samaki Mei,20,2020 hadi Juni 14,2020 tayari imeshasafirisha minofu ya Samaki nje ya nchi takriban  tani 147 ambapo amesema hali hiyo imeendelea vizuri katika kuinua uchumi wa nchi.
Kuhusu changamoto za usafirishaji wa minofu ya samaki Mhandisi Kamwelwe amesema wameshaanza kuzifanyia kazi zikiwemo uingizaji wa minofu ya samaki kwenye ndege ulikuwa ukichukua muda mrefu.
Kikao kazi hicho cha wadau wa sekta ya Samaki kimelenga Zaidi kuinua soko la samaki   hapa nchini ambapo usafirishaji wa minofu ya samaki umekuwa na tija kubwa tangu uboreshaji wa usafirishaji uanze kuboreshwa.

Post a Comment

0 Comments