TANGAZA NASI

header ads

Tanesco Bagamoyo yawataka wananchi kuachia eneo la Ukuni



Na Omary Mngindo, Bagamoyo
Juni 22

WANANCHI waishio Kitongoji cha Ukuni Kata ya Dunda Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wanaojihusisha na kilimo eneo la Shirika la Umeme nchini Tanesco, kutolitumia tena eneo hilo baada ya kumaliza kuvuna.

Eneo hilo lililopo jirani kabisa na mzunguko wa barabara itokayo Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo na Msata, linamilikiwa na Shirika hilo ambapo kwa kipindi kirefu sasa linatumiwa na wakazi kwa ajili ya kilimo cha mpunga, hivyo kuliachia baada ya kuvuna.

Hayo yalielezwa na Meneja wa shirika hilo wilaya hapa Daniel Kyando, akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo alisema kuwa eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya shughuli za kushusha nguzo kabla ya kusambazwa maeneo mbalimbali.

"Nitumie fursa hii kuwaasa wateja wetu wanaolima mpunga katika eneo la Shirika pale Kitongoji cha Ukuni, jirani kabisa na mzunguko wa magari yanayotokea Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo mjini na Msata, mara baada ya kuvuna mpunga tunawaomba waliachie tunataka kuweka nguzo," alisema Kyando.

Aliongeza kuwa kwa sasa wameamua kuwaachia ili wamalizie kuvuna mazao yao, na kwamba mara baada ya zoezi hilo wasilitumie tena kwa ajili ya kulima kwani wataanza rasmi kuweka nguzo ambazo kwa sasa wameziweka kwa muda kwenye shule ya msingi ya  Mbaruku iliyoko Kitongoji cha Mwanakalenge.

"Tunawaandikia barua Mwenyekiti na Mtendaji wa eneo husika kuwataarifu juu ya hatua hiyo ya kuwataka wateja wetu wanaolima mpunga jirani na njiapanda ya barabara itokayo Dar es Salaam kuingia Bagamoyo mjini na nyingine upande wa Msata," alisema Kyando.

Mmoja wa wananchi wanaojishughulisha na kilimo katika eneo hilo akijitambulisha kwa jina la Mwajuma Issa aliushukuru uongozi wa Tanesco kwa kuwajulisha mapema juu ya hatua hiyo, na kwamba wameelewa na watazingatia maelekezo.

"Binasfi nashukuru kwa taarifa hii matumaini yangu ni kwamba wenzangu wote watakuwa wameelewa, ukijumlisha na vyombo vya habari ikotoka imani yangu ujumbe utawafikia wote, na barua itayofika kwa viongozi wetu itaongeza elimu kwetu," alisema Mwajuma.


Post a Comment

0 Comments