TANGAZA NASI

header ads

Kugombea Ubunge Kyela ilikuwa uamuzi mgumu- Mwakyembe


Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akiongea kupitia Sports HQ EFM amesema moja kati ya maamuzi magumu aliyowahi kufanya maisha mwake, ni kuachana na Ubunge wa Afrika Mashariki na kwenda kugombea huko Kyela.

"Mimi nilikuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Bunge ambalo halina patashika.....unaacha dola elfu kadhaa unaenda kupewa laki 9 kwa wakati ule" alisema Dkt Mwakyembe na kusema kwamba ilibidi akagombee kutokana na ushawishi wa viongozi wake.

Hata hivyo amesema anashukuru kwani baada ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Kyela, jimbo hilo limepata maendeleo yanayoonekana. .

Post a Comment

0 Comments